Tuko Pamoja

Tuko Pamoja

Monday, June 15, 2015

MBUNGE JOSEPH MBILINYI ALIPOHUDHURIA SHEREHE YA KIMILA YA WASAFWA

  • ILIHUSISHA MKUSANYIKO WA MACHIFU WOTE WA KABILA HILO
  • PICHANI CHIFU MKUU MWANSHINGA AKIMSIKILIZA MBUNGE


MBUNGE JOSEPH O. MBILINYI ANASOMESHA KUPITIA MFUKO WA ELIMU

( muendelezo wa SUGU NA ELIMU - 2 )..... 

Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph O. Mbilinyi "Sugu" anasomesha wanafunzi katika shule mbalimbali za sekondari, na hii ilitokana na baada ya kuanza kazi ya Ubunge moja ya changamoto aliyokumbana nayo ni wingi wa walezi na wanafunzi waliofika ofisini au waliomuona  kwa ajili ya kuomba msaada wa kusaidiwa ada na gharama nyingine za shule, ndipo ikapelekea aanzishe Mbeya Education Trust Fund (METF) au Taasisi ya Mfuko wa Elimu Mbeya.

Ambapo taasisi hii METF katika moja ya jukumu lake imeweza kusaidia wanafunzi wa sekondari  takribani 270 waliofaulu na hawakuwa na uwezo kutokana na  kuwa wanatoka kwenye familia zenye uwezo mdogo kiuchumi kwa kuwalipia ada na sare za shule pamoja na mahitaji mengine ya elimu pale inapobidi, na ilipoanza mwaka 2013 ilianza na watoto wa kidato cha 1 mpaka 4 (o'level) lakini sasa imeweza kusaidia mpaka wanafunzi wa kidato cha 5 na 6 (A level).

Imetolewa na  OFISI YA MBUNGE MBEYA MJINI

(Chini ni picha mbalimbali za baadhi ya watoto wanaosomeshwa na Mfuko  huu wakiwa na Afisa wa METF)




Sunday, June 14, 2015

MBUNGE "SUGU" AIBUKIA KISIWANI MAFIA

• AFANIKIWA KUTOA VIONGOZI WA CHADEMA POLISI
• ATEMBELEA VIJIWE NA KUFANYA MKUTANO WA HADHARA


Mbunge wa Mbeya Mjini kupitia CHADEMA Joseph O. Mbilinyi "Sugu" wikiendi hii alikuwa kwenye ziara ya ujenzi wa Chama kwenye kisiwa cha Mafia na kufanikiwa kufanya mambo kadha wa kadha ya ujenzi wa Chama. 

Katika ziara yake hiyo ambayo licha ya kutembelea vijiwe mbalimbali na kubadilishana mawazo na wakazi wa kisiwa hicho pia alikumbana na mkasawa kushikiliwa kwa viongozi wa CHADEMA kisiwani hapo kwa makosa yasioeleweka ambapo kikosi hicho cha Mbunge huyo wa Mbeya waliweza kupigania mpaka usiku wa manane kuhakikisha viongozi hao wanatolewa polisi.

Pia katika ziara hiyo Mbunge pia aliweza kuongea na viongozi wa Kata katika jimbo hilo la Mafia pamoja na kusalimiana na vijana wa kikosi cha Red Brigade katika kisiwa hicho pamoja na kusaini kadi nyingi za CHADEMA ambazo wakazi wa kisiwa hicho walikuwa wakizihitaji kwa udi na uvumba. 

Baadaye jumapili aliweza kuongea na wakazi wa kisiwa hicho kupitia mkutano wa hadhara uliofanyika kisiwani hapo na kusisitiza elimu ya uraia ikiwemo kutoogopa vitisho vya polisi ambao ni vibaraka wa chama tawala.

Mbunge huyo pia alivutiwa na mandhari tulivu ya kisiwa hicho na huku akiwa amefikia katika chumba ambacho akina AC wala TV ambapo kwa madai yake alisema ni kizuri kwa utulivu na kutafakari.













KUTOKA OFISI YA MBUNGE MBEYA MJINI..... (SUGU NA ELIMU - 1)

IJUE PROGRAMU YA KOMPYUTA MASHULENI

Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph O. Mbilinyi anaendesha programu ya mafunzo ya kompyuta kwa wanafunzi wa sekondari za Kata zilizopo jijini Mbeya ambapo tayari ameanzisha madarasa ya kompyuta katika shule za sekondari tano (5)  kati ya 10 ambazo zitafikiwa na mradi huu kwa  awamu ya kwanza, shule hizo ni Shule ya Sekondari Mwakibete, Shule ya Sekondari Uyole, Shule ya Sekondari Forest, Shule ya Sekondari Iwambi na Shule ya Sekondari Iganzo. 

Lengo la programu hii ni kuhakikisha wanafunzi wa shule za Mbeya wanapomaliza kidato cha nne (4) wawe na uwezo wa kutumia kompyuta hali iliyopelekea kuongeza hadhi za shule na elimu kwa ujumla katika shule za Kata jijini Mbeya









Friday, August 8, 2014

SUGU AWALAUMU POLISI KURUSHA MABOMU MBEYA

Mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ amelishutumu Jeshi la Polisi mkoani humo kuwa ndiyo chanzo cha vurugu baada ya juzi kutumia mabomu ya machozi kuwazuia wafuasi wa Chadema na waombolezaji kuubeba mikononi mwili wa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Itiji,  Ezekiel  King kwa lengo la kutembea nao kwa miguu kutoka Hospitali ya Rufaa Mbeya hadi nyumbani kwake Itiji kuuzika.
Baada ya mabomu hayo kurushwa, viongozi na waombolezaji walilazimika kulibwaga chini jeneza la mwili wa marehemu na kuanza kukimbia.
Marehemu alifariki dunia katika hospitali hiyo, alikopelekwa  kwa ajili ya matibabu baada ya kuugua ghafla katika Gereza la Ruanda alikokuwa akitumikia kifungo cha miaka saba baada ya kupatikana na kosa la kudhuru mwili wa mwanachama wa CCM .
Akizungumzia tukio hilo, Sugu alisema kilichotokea juzi ni uthibitisho kwamba polisi ndiyo wamekuwa chanzo cha vurugu.
“Sisi tulikuwa kwenye msafara wakaja kutuzuia na kuninyooshea bunduki. Tukawaeleza tunakwenda kuzika, wao wanasema tulitakiwa kuomba kibali cha kwenda kuzika,” alisema Sugu na kuongeza: “Watu walikuwa wengi na magari ya kuwabeba kwenda kuzika hayakuwepo, tuliamua kutembea sasa kibali cha nini,” alisema Sugu.

Sugu alisema polisi wasipobadilika mara moja, wananchi watachukua hatua kuwaondoa katika nyumba walizopanga uraiani ili wakaishi kituo kikuu cha polisi mkoani humo kwa vile hawaijali jamii inayowazunguka.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi aliwataka Chadema kuacha kuwazushia polisi na kuongeza kuwa madai ya Sugu hayana ukweli wowote.
  • Mwandishi Wetu, Mwananchi

Thursday, August 7, 2014

MBUNGE JOSEPH MBILINYI AKABIDHI VIFAA VYA CHAMA KWA BAVICHA JIJINI MBEYA

  • KATIBU WA MBUNGE KWAME ELLY ANANGISYE AMKABIDHI MWENYEKITI BAVICHA MBEYA MJINI  MOSES MWAIFUNGA KWA NIABA YA MBUNGE 
 

POLISI MBEYA WAFYATUA MABOMU NA KUPORA JENEZA MBELE YA MBUNGE JOSEPH MBILINYI "SUGU"

  • NI LA MAREHEMU KING ALIYEKUWA MWENYEKITI  SERIKALI YA MTAA ITIJI
  • ALIFIA GEREZANI ALIKOKUWA ANATUMIKIA KIFUNGO CHA MIAKA 7
  • RUFAA YA KESI YAKE YENYE UTATA ILIKUWA ISIKILIZWE TAR. 11/8/2014


 
 
  •